You are currently viewing EDDY KENZO AJUTIA KUMPIGA SHABIKI NA MIC, AOMBA RADHI

EDDY KENZO AJUTIA KUMPIGA SHABIKI NA MIC, AOMBA RADHI

Mwanamuziki kutoka Uganda Eddy Kenzo amewaomba radhi mashabiki zake kwa kufeli kudhibiti hasira yake kwenye onesho lake huko Bwera, Kasese.

Kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Kenzo anaonekana akimrushia shabiki kipaza sauti kwa madai ya kumwagia kinywaji akiwa jukwaani.

Kenzo amesema kinywaji hicho kilikuwa kimechanganywa na kilevi na harufu yake mbaya ndio ilimfanywa akapandwa na hasira.

Licha ya kuwa alisema kwamba hajutii kitendo cha kumpiga shabiki na kipaza sauti, msanii huyo ameamua kuwaomba radhi mashabiki zake akisema kuwa anajutia maamuzi aliyoyachukua ikizingatiwa kuwa yeye ni kioo cha jamii.

“My fans expect better from me. I know and I regret my actions. I think this guy was sent by people who want to taint my image, but it’s fine. I forgive him,” says Eddy Kenzo.

Utamkumuka Septemba mwaka wa 2014 Kenzo alimshushia kichapo cha mbwa mtangazaji wa Dembe FM Isaac Katende maarufu kama Kasuku kwenye mkao na wanahabari huko Centenary Park kwa madai ya kumzungumzia vibaya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke