You are currently viewing Eddy Kenzo akanusha kuwa muumini wa dhehebu la Illuminati

Eddy Kenzo akanusha kuwa muumini wa dhehebu la Illuminati

Msanii nyota kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo amenyosha maelezo kuhusu madai ya kutumia ishara ya illuminati kwenye video ya wimbo wake “Semyekozo”..

Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema alama alizozitumia kwenye video ya wimbo huo haihusiani kabisa na nguvu za kishetani kama baadhi ya walimwemgu walivyohoji mtandaoni kwani ni ishara ya kawaida ambayo watu hutumia kwenye maisha ya kila siku mitaani.

Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amewataka watu waache kuwa na fikra za kishamba kwa kuwahusisha watu wenye mafanikio na nguvu za giza huku akisema kuwa chimbuko la illuminati limetokana na makundi ya watu matajiri duniani na sio madhehebu ya kishetani kama wengi wanavyodhani.

Utakumbuka miaka kadhaa iliyopita baada ya Eddy Kenzo kutusua kimataifa, walimwengu walihoji kuwa huenda utajiri na mafanikio yake kisanaa imetokana na hatua yake kuingia ubia wa kufanya kazi na dhehebu la illuminati.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke