You are currently viewing EDDY KENZO AKASHIFU VIKALI MUUNGANO WA WASANII NCHINI UGANDA

EDDY KENZO AKASHIFU VIKALI MUUNGANO WA WASANII NCHINI UGANDA

Mwanamuziki Eddy Kenzo amekashifu uongozi wa Muungano wa Wanamuziki nchini Uganda (UMA), akiwataja kuwa matapeli.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Kenzo ambaye anafanya vizuri na singo yake mpya “Nsimbudde” amedai kuwa viongozi wa Muungano Wanamuziki chini Uganda wamekwenda kinyume na malengo ya kubuniwa kwake kwani wamegeuza muungano huo kuwa kitega uchumi ya kuwanufahisha watu wachache huku wasanii wakiendelea kuishi maishi ya uchochole.

“Nilikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa na imani kubwa na UMA lakini walipoteza mweelekeo. Sasa inahusu pesa, sio tasnia ya muziki tena,” alifafanua Eddy Kenzo.

Bosi huyo wa Big Talent ameongeza kuwa hana tena kadi ya uanachama wa UMA na hatashiriki katika uchaguzi ujao wa muungano huo.

Kauli ya Eddy Kenzo imekuja mara baada ya rais wa sasa wa muungano huo Cindy Sanyu kudai kuwa uchaguzi wa kuwachagua viongozi  wapya utafanywa kwa njia ya mtandao kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha.

Utakumbuka muungano wa wanamuziki nchini uganda unatarajiwa kuundaa uchaguzi wa kuwateua viongozi wapya wa muungano huo mwezi Mei mwaka huu na tayari tumeona wasanii kama Cindy Sanyu, King Saha na Maurice Kirya wamejitoza kuwania wadhfa wa urais huku Daddy Andre na Kalifah Aganaga wakitarajiwa kuchuana kwenye wadhfa wa Unaibu wa rais.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke