You are currently viewing EDDY KENZO AKATAA KUZUNGUMZIA MPANGO WA KUTOA MATUNZO KWA BINTI YAKE NA REMA NAMAKULA

EDDY KENZO AKATAA KUZUNGUMZIA MPANGO WA KUTOA MATUNZO KWA BINTI YAKE NA REMA NAMAKULA

Bosi wa Big Talent, Msanii Eddy Kenzo hayuko tayari kujibu maswali yoyote kuhusiana na mpango wake wa kutoa matunzo kwa binti yake aliyezaa na msanii Rema Namakula.

Akizungumza na Spark TV, Eddy Kenzo ameeleza kuwa haimkalii vizuri kuzungumzia masuala yake ya faragha hadharani huku akisema kwamba anamheshimu sana binti yake, hivyo hapendi watu wakimjadili mtandaoni.

Eddy Kenzo ametoa kauli hiyo mara baada ya kuulizwa upande wake wa stori kufuatia hatua ya baby mama wake Rema Namakula kusema kwamba wanashirikiana vyema na mkali huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” kwenye suala la kutoa mahitaji ya msingi kwa binti yao.

Utakumbuka Rema Namakula aliachana na Eddy Kenzo mwaka wa 2019 ambapo aliingia kwenye mahusiano mengine na Dakta Hamsa Ssebunya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke