Nyota wa muziki nchini Uganda Eddy Kenzo amejiunga na orodha ya mastaa ambao wanakosoa mchakato uliotumika kuaandaa tuzo za Janzi Awards zilizokamilika majuzi nchini humo.
Katika mkao na wanahabari Eddy kenzo amewataka wanahabari kuwaweka waandaji wa tuzo za muziki nchini uganda kwenye mizani kama njia ya kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili tasnia ya muziki nchini humo.
Hitmaker huyo wa “Leero Party” amewatolea uvivu wanaotilia shaka ushindi wake kwenye tuzo za Afrimma mwaka 2021 kwa kusema kwamba hatotishia na maneno yao kwenye mitandao ya kijamii kwani anafahamu fika alistahili kupewa tuzo ya msanii bora wa kiume kutokana na kazi zake za muziki.
Ikumbukwe kwa wiki kadhaa sasa baadhi ya wasanii nchini uganda wakiongozwa na Spice Diana wamekuwa wakiwarushia lawama waandaji wa tuzo za Janzi Awards kwa kutokuwa na uwazi kwenye tuzo hizo.