Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo ameingia ubia wa kufanya kazi na Mamlaka ya Wanyama pori nchini Uganda UWA kwa ajili ya kutangaza mbuga za wanyama kimataifa
Eddy Kenzo amelamba dili hilo nono wiki moja iliyopita na sasa anaendelea na harakati za kuaandaa maudhui yatakayotumiwa kutangaza utalii nchini Uganda duniani.
Utakumbuka kipindi cha nyuma Eddy Kenzo amefanya kazi kama balozi wa utalii nchini Uganda na Kenya mtawalia.
Eddy kenzo ni moja kati ya wasanii wanaotangaza muziki wa Uganda na Afrika Mashariki kimataifa shukran kwa wimbo wake Sitya Loss ambayo ilimfungulia milango mwaka wa 2014.