Msanii Eddy Kenzo amehapa kwamba hatokuja kumvunjia heshima Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa lengo la kuwafurahisha wapinzani wake.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Kenzo ambaye juzi kati aliteuliwa kuwania tuzo ya Grammy 2023 kupitia kipengele cha Best Global Perfomance, amekiri kuwa Museveni ni mwokozi wake kwani alikuwa mtu wa msaada kwake kipindi cha korona alipofungiwa nchini Ivory Coast.
“I will never abuse Museveni to make his opponents happy. That is what they want but his my saviour. He saved me during the pandemic,” alisema.
Kauli yake imekuja mara baada ya wafuasi wa chama cha NUP inayoongozwa na Bobi Wine kumkashifu kwa hatua ya kujihusisha na viongozi wakuu serikalini kwenye tamasha lake lilomalizika wikiendi iliyopita huko Kololo Airstrip.
Utakumbuka mapema wiki hii Eddy Kenzo alidai kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya watu wasiojulikana kuanza kumtolea vitisho vya kumuangamizi.