Bosi wa Big Talent, Eddy Kenzo ametangaza kumuunga mkono msanii mwenzake King Saha kwenye azma yake kuwania urais wa chama cha wanamuziki nchini uganda UMA.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amethibitisha kuwa atampigia kura King Saha kama Rais ajaye wa Chama cha (UMA) akisema kwamba msanii huyo anaelewa matatizo ya yanayokumba tasnia ya muziki nchini uganda, kwani atawatumikia wanamuziki vyema.
“King Saha alinipigia simu na kuniomba nimpigie kura ya kuwa rais wa UMA, pia nilianza muziki na King Saha, nakumbuka enzi zile tulikuwa studio tukishauriana, kipindi hicho hakuna aliyemfahamu, hivyo namuelewa sana. Siwezi kumsaliti, “alisema.
Hata hivyo King Saha amemshukuru Mfalme Eddy Kenzo kwa kubali wito wake wa kuwasimamia wasanii wa uganda kupitia cha UMA.