Staa wa muziki kutoka Uganda Eddy Kenzo ameamua kumsaidia msanii mwenzake Clever J baada ya ndugu zake kumtelekeza.
Eddy kenzo ambaye juzi kati alitumbuiza pamoja na Clever J kwenye show ya Comedy Gate, aliamua kumpa msanii huyo pesa zote alizopewa na mashabiki kama njia ya kumsaidia kijikwamua kimaisha.
Hatua hiyo ya Eddy kenzo wengi wametafsiri kama kejeli kwa ndugu zake Chameleone na Pallaso ambao wamekuwa wakitumia jina la Clever J kujipatia pesa.
Clever J anatarajiwa pia kutumbuiza kwenye tamasha la Eddy Kenzo mwezi Novemba mwaka huu kama njia ya kujipatia kipato ya kujiendeleza kimaisha.