You are currently viewing EDDY KENZO AMTWANGA SHABIKI NA KIPAZA SAUTI HADI AKAPOTEZA FAHAMU.

EDDY KENZO AMTWANGA SHABIKI NA KIPAZA SAUTI HADI AKAPOTEZA FAHAMU.

Mwanamuziki kutoka Uganda Eddy Kenzo ameingia kwenye vichwa vya habari Afrika Mashariki mara baada ya kuripotiwa kumtwanga na kipaza sauti shabiki yake mmoja kwenye moja ya show yake juzi kati.

Inasemekana kuwa nguvu ya kipaza hiyo ilitosha kumuangusha chini shabiki huyo ambaye alibamiza kichwa chini baada ya kuanguka na kulala kabla ya walinzi wa Eddy Kenzo kumkamata na kumtupa nje ya ukumbi ambao msanii huyo alikuwa akitoa burudani.

Inadaiwa kuwa chanzo cha purukushani hiyo ni baada ya shabiki huyo kumwagia kinywaji Eddy Kenzo alipokuwa jukwaani akitumbuiza wimbo wake wa Enjoyment, kitendo ambacho kilimkasirisha msanii huyo ambaye yupo kwenye ziara ya kimuziki na kuamua kumrushia kipaza sauti.

Utakumbuka hii sio mara ya kwanza kwa Eddy Kenzo kujipata kwenye msala kama huo, amewahi pia kumzaba makofi mtangazaji mmoja wa redio nchini Uganda baada ya kumharibia jina kwa kusema kwamba Eddy Kenzo sio msanii mwenye kipaji kwani aliandikiwa wimbo wake uitwao Syemkozi na prodyuza aitwaye Ronnie, madai ambayo mwanamuziki huyo alikanusha vikali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke