Msanii nyota kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo anataka kila aliye karibu yake afanikiwe, amehamua kumpa maua yake Martha Mukisa akiwa hai.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Weekend” kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni amemsifia Martha Mukisa kwa kusema kwamba anapenda jinsi anavyofikiri lakini pia ubunifu wake kwenye muziki.
Eddy Kenzo amesema Martha Mukisa amemempa moyo wa kuwasaidia wasanii chipukizii nchini uganda kupitia lebo yake ya muziki ya Big Talent Entertaintment.
Martha Mukisa amekuwa akisuasua kimuziki kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini nyota yake ilikuja ikang’aa mwaka wa 2021 alipofanya wimbo wa pamoja na Eddy Kenzo uitwao Sango.
Utakumbuka Eddy Kenzo na Martha Mukisa wana ukaribu sana jambo ambalo limewafanya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa ni wapenzi.