You are currently viewing Eddy Kenzo ashtakiwa na Promota kwa kukiuka mkataba wa kufanya tamasha la muziki

Eddy Kenzo ashtakiwa na Promota kwa kukiuka mkataba wa kufanya tamasha la muziki

Mwanamuziki Eddy Kenzo ameburuzwa mahakamani kwa kufanya tamasha la muziki wikiendi iliyopita bila kumhusisha promota muziki nchini humo Luba Events.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Luba amewasilisha kesi mahakamani kumzuia msanii huyo haziweze kufanya matamasha ya muziki nchi Uganda hadi pale uamuzi wa kesi yake itakapotolewa.

Promota huyo amedai kuwa alisaini mkataba wa kufanya onesho la muziki na Eddy Kenzo mwaka 2020 ambapo alienda mbali zaidi na kumlipa Ksh 3.9 millioni lakini wakati janga la Corona lilizuka walilazimika kuahirisha onesho lao.

Luba amesema licha ya kumuandika Eddy Kenzo barua ya kumuonya asifanye tamasha hilo la muziki bila kumshirikisha, msanii huyo alikwenda kinyume na agizo lake na kufanya tamsha hilo mwenyewe.

Hata hivyo amedai kuwa jaribio la kutatua sakata lake na Eddy Kenzo halikuzaa matunda, jambo ambalo lilimlazimu kumfungulia kesi mahakamani.

Ikumbukwe Luba Events alikuwa miongoni mwa mapromota wa muziki waliofidiwa na serikali ya Uganda kwa hasara waliyopata wakati wa janga la Corona baada ya matamasha ya muziki kusitishwa ghafla.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke