Bosi wa lebo ya muziki Big Talent Eddy Kenzo amejiunga na orodha ya wasanii kutoka nchini Uganda wanaotaka kuacha tasnia ya muziki.
Katika mahojiano yake wiki hii , Kenzo ameelezea nia yake ya kuacha kabisa biashara ya muziki na kwenda kujikita kwenye kilimo huko Masaka nchini Uganda.
Eddy Kenzo, ambaye amepata mafanikio mengi kwenye muziki wake amesema anataka kusahau kila kitu kuhusu muziki na kuanza kuishi maisha ya utulivu.
Hitmaker huyo wa “Sango” amedokeza atakuwa anatumbuiza mara moja baada ya muda huku akielekeza nguvu zake zote kwenye biashara nyingine ambazo zitamuingiza kipato.
Ikumbukwe juzi kati msaniii Winnie Nwagi pia alikiri kuwa amechoshwa na tasnia ya muziki nchini Uganda kutokana na wa kukosoa vikali kwenye mitandao ya kijamii.