Bosi wa Big Talent, Msanii Eddy Kenzo amewashauri vijana kujiepusha na ndoa za mapema.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amedai kuwa vijana wanapaswa kueleza nguvu zao kwenye masuala ya kujiboresha kiuchumi kabla ya kuingia kwenye ndoa.
“Nawashauri vijana kuchukua muda wao kabla ya kufunga ndoa. Nimekuwepo na nazungumza kutokana na uzoefu,” alisema.
Awali Eddy Kenzo alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii Rema Namakula ambaye wamejaliwa kumpata mtoto mmoja lakini wawili hao walikuja wakatengana mwaka 2019 na tangu wakati huo mshindi huyo wa BET hajawahi kuingia kwenye mahusiano mengine.