You are currently viewing EDDY KENZO AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

EDDY KENZO AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

Msanii Eddy Kenzo amewahimiza wasanii wenzake nchini Uganda kutowaingilia wasanii wa Nigeria ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye soko la muziki duniani.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema muziki wa nigeria umepata mapokezi mazuri kwa sababu ni wakati wao kung’ara huku akiwataka wasanii wa uganda kutia bidii kwenye kazi zao kwani kuna kipindi muziki wao pia utafanya vizuri duniani akitolea mfano muziki wa Congo na Jamaica ambao umepotea kwa sasa licha ya kupata mapokezi makubwa miaka ya hapo nyuma.

“They are trending in the whole world because that’s how their music is performing. It’s just their season, and we shall also get ours. Even Congolese and Jamaicans dominated our airways years back but they are no more,” Alisema.

Hitmker huyo wa “Follow” amesema wasanii wa nigeria wamewekeza pesa nyingi kwenye muziki wao kiasi cha kuwa na mawakala nchini uganda ambao wanawalipa madeejay kucheza nyimbo zao.

“Nigerians invest so much money in their music and promotion. They have agents here and they pay deejays to play their music,” Aliongeza.

Hata hivyo amesema wasanii hao wanapaswa kulipwa pesa nyingi kwenye shows zao kwa sabababu wametumia pesa nyingi kutengeneza brand zao za muziki tofauti na wasanii wa Uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke