Msanii Eddy Kenzo ametoa changamoto kwa wanamuziki nchini kwao Uganda kuendelea kufanya muziki wao wa asili uitwao Kandogo Kamu.
Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amewataka wasanii kufuata nyayo za wakongwe waliokuwa wanafanya mtindo huo wa muziki bila kukataa tamaa, kipindi muziki wa Congo ulikuwa umekita mizizi nchini Uganda miaka ya hapo nyuma.
Bosi huyo wa Big Talent amesema wasanii wa Uganda wakiaanza kurekodi nyimbo zenye mahadhi ya Kandongo Kamu wanaweza uwezo mkubwa wa kushindana na wanamuziki wengine duniani
Eddy Kenzo kwa sasa yupo kwenye matayarisho ya tamasha lake la muziki ambalo linatarajiwa kufanyika Novemba 12 mwaka 2022.