You are currently viewing EDDY YAAWE AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU WIMBO WA NETEZE ALIOMSHIRIKISHA MARTHA MUKISA

EDDY YAAWE AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU WIMBO WA NETEZE ALIOMSHIRIKISHA MARTHA MUKISA

Mwimbaji mkongwe kutoka Uganda Eddy Yaawe amekanusha madai kwamba alitaka wimbo wa “Neteze” aliomshirikisha martha mukisa uwe kwenye Youtube channel yake ili afaidi na mirabaha ya wimbo huo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Eddy Yaawe amepuzilia madai hayo kwa kusema kwamba hajawahi pata pesa zozote kutoka kwenye channel yake ya youtube na uvumi huo unaosambaa mtandaoni kwa sasa ni njia ya uongozi wa Martha Mukisa kumtangaza msanii wao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Love Yo” ameshikilia kuwa uhusiano wake na Martha Mukisa ungali mzuri licha ya kutokuwa na maelewano mazuri katika pindi cha wiki chache zilizopita.

Kauli ya Eddy Yaawe imekuja mara baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Uganda kudai kwamba msanii huyo alifuta collabo yake na Martha mukisa kwenye mtandao wa youtube kwa sababu alitaka anufaike na mirabaha ya wimbo huo mwenyewe.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke