You are currently viewing Eddy Yawe afunguka kuwanyanyasa kimapenzi wasanii wa kike

Eddy Yawe afunguka kuwanyanyasa kimapenzi wasanii wa kike

Mwimbaji wa zamani wa bendi ya Afrigo Eddy Yawe ameamua kuvunja kimya chake kuhusu tuhuma za kuwanyanyasa kimapenzi wasanii wa kike.

Katika mahojiano yake hivi karibu Yawe amesema tuhuma zote alizozushiwa mtandaoni hazina ukweli wowote kwani ilikuwa njia ya baadhi ya watu kumshusha kimuziki

Msanii huyo kutoka nchini Uganda amenyosha maelezo kuhusu ugomvi wake na Msanii Carol Nantogo akisisitiza kuwa chanzo cha kukosana kwao ni hatua ya mrembo huyo kudhani kuwa ilikuwa lazima watumbuize pamoja wimbo wao “Tukiggale” kila sehemu anayopata mwaaliko.

Lakini ameeleza kuwa walikuja wakatatua tofauti zao baada ya Nantogo kumuomba msamaha na sasa wana uhusiano mzuri kikazi.

Hitmaker huyo “Love Yo” amezungumzia pia suala la kutokuwa na maelewano mazuri na msanii Martha Mukisa kwa kusema kuwa utofauti wao uliibuka kutokana na masuala ya hakimiliki wa wimbo wao “Neteze” na sio kumnyanyasa kingono kama ilivyoripotiwa mtandaoni kwani madai hayo yaliibuliwa na watesi wake.

Hata hivyo kuhusu sakata la kumdhulumu kimapenzi msanii chipukizi Sheebah Sumayiyah Eddy Yawe amesema suala hilo linatatuliwa faraghani na hivi karibuni sheria itafuata mkondo wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke