You are currently viewing EDDY YAWE AJUTIA KUJIUNGA NA SIASA, AKIRI KUPOTEZA PESA NYINGI

EDDY YAWE AJUTIA KUJIUNGA NA SIASA, AKIRI KUPOTEZA PESA NYINGI

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Eddy Yawe amekiri kujutia uamuzi wake wa kujiunga na siasa.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Eddy Yawe amesema hajafaidi kivyovyote na siasa licha ya kuwekeza pesa nyingi kwenye azma yake kuwa meya wa manispaa ya Kira nchini Uganda.

Ikumbukwe Eddy Yawe kwenye mahojiano yake mbali mbali amekiri kuwa aliuza mali yake nyingi kwa ajili ya kufadhili kampeini zake za kisiasa kitu ambacho amekuwa akijutia kwani amepoteza pesa nyingi.

Eddy Yawe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2021 nchini alijaribu kumuondoa mamlakani meya wa sasa wa Manispaa ya Kira nchini Uganda lakini hakufanikiwa kumng’atua afisini.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke