Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Eddy Yawe ametoa wito kwa msanii mwenzake Catherine Kusasira kujiunga na chama cha NUP kinachongozwa na Bob Wine.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Eddy Yawe amesema kama kweli Kusasira amechoshwa na chama tawala cha NRM,itakuwa ni jambo la busara kwa msanii huyo kujiunga na NUP, chama ambacho kinapigania demokrasia nchini Uganda.
Kauli ya Eddy Yawe imekuja mara baada ya Catherine Kusasira kukiri hadharani kuwa Chama cha NRm kimemtelekeza licha ya kuingia kifua kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2021, hivyo anafikiria kujiondoa kwenye chama hicho.
Utakumbuka mwaka wa 2021 Catherine Kusasira alimkashifu Bob Wine hadharani kwa hatua ya kushindana na Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini Uganda.