Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Eddy Yawe amekanusha madai ya kumnyanyasa kimapenzi msanii wa kike nchini humo Martha Mukisa.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Yawe amesema madai hayo hayana ukweli wowote huku akisisitiza kwamba uhusiano wake na Martha Mukisa ulikuwa wa kikazi tu.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Love Yo” amesema walitafautiana kimawazo na Martha Mukisa wakati uongozi wake ulitaka kuchukua wimbo wake Neteze kwa nguvu bila ridhaa yake kwa kumnyima haki za umiliki wa wimbo huo walipopakia kwenye akaunti ya Youtube ya mrembo huyo.
Kauli ya Eddy Yawe imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa ugomvi kati yake na Martha Mukisa kuhusu umiliki wa wimbo wa Neteza ulitokana na mrembo huyo kukataa kutoka nae kimapenzi.