You are currently viewing EDDY YAWE ATUHUMIWA KUMNYANYASA KINJISIA MSANII CHIPUKIZI UGANDA

EDDY YAWE ATUHUMIWA KUMNYANYASA KINJISIA MSANII CHIPUKIZI UGANDA

Msanii Eddy Yaawe ameingia kwenye headlines mtandaoni mara baada ya msanii mwenye asili ya Uganda anayeishi nchini Denmark kumkashifu kwa madai ya kuhujumu shughuli zake za muziki.

Msanii huyo anayefahamika kwa jina la Sumaya Sheebah amefunguka na kudai kuwa Eddy Yawe aliuuza wimbo wake kwa mtu mwingine bila ridhaa yake alipokataa kumpa rushwa ya ngono.

Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa licha ya kukubali kulipia gharama zote za kuandaa na kutayarishaji video ya wimbo huo, Eddy Yawe aliamua kufanya kazi hiyo na msanii mwingine aitwaye TYBA.

Sheebah amedai alikutana na bosi huyo wa Dream Studios mwaka wa 2017 huko Copenhagen ambako walitia sahihi mkataba wa kufanya kazi pamoja ila tangu kipindi hicho amekuwa akimpa ahadi za uongo

Hata hivyo Eddy Yawe amesalia kimya kuhusu tuhuma hizo za kutaka kimnyanyasa kinjisia binti huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke