Mkongwe wa muziki kutoka nchini uganda Eddy yawe ametoa changamoto kwa wasanii kutia bidii kwenye kazi zao za muziki ili waweze kutimiza malengo yao maishani.
Yawe ambaye ni kaka wa bobi wine amesema kiwanda cha muziki nchini uganda kina fedha nyingi hivyo wasanii wanapaswa kujenga tabia ya kuweka akiba badala ya kutumia pesa zao zote kwenye starehe..
Kauli ya Eddy yawe imekuja mara baada ya kukamilisha ujenzi wa mjengo wake wa kifahari uliomgharimu takriban shillingi millioni 155 viungani mwa jiji la kampala.
Licha ya Eddy Yawe kusisitiza kwamba ni bidii yake ndio imechangia kukamilisha mjengo wake wa kifahari baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanahoji kwamba mradi wake huo ulifadhiliwa na serikali.