Carol Nantongo and msanii mkongwe nchini Uganda Eddy Yawe walitubariki na smash hit yao iitwayo “Tukigale” mwaka wa 2018.
Wimbo huo ulifanya vizuri sokoni lakini wawili hao walikuja wakaiingia kwenye ugomvi kutokana na umiliki wake wa Tukigale kiasi cha kutotumbuiza wimbo huo kwenye matamasha mbali mbali ya muziki.
Hata hivyo wikiendi hii iliyopita wawili hao walikutana jukwaani na wakatumbuiza pamoja wimbo wa Tukigale kwenye hafla moja ya harusi ambayo walialikwa kutoa burudani.
Eddy Yawe na Carol Nantongo walionekana wakikumbatiana jukwaani kabla ya kuwaambia mashabiki zao kuwa wameweka tofauti zao kando kuhusu umiliki wa wimbo huo.
Utakumbuka juzi kati Eddy Yawe walizozana na msanii mwenzake Martha mukisa baada ya kuachia kolabo yao itwayo Neteze.