Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Eddy Yawe ameingia kwenye ugomvi na msanii chipukizi nchini humo Martha Mukisa kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao “Neteze”.
Hii ni baada ya Eddy Yawe kufuta wimbo huo kwenye akaunti ya youtube ya msanii Martha Mukisa kwa kigezo kuwa wimbo wa “Neteze” ni wake.
Kulingana na Eddy Yawe yeye ni ndio mmiliki halisi wa wimbo huo kwani aligharamia pesa zote za kutayarisha audio pamoja na video
Hata hivyo chanzo cha karibu na Martha Mukisa kinadai kuwa msanii hyuo anaamini kwamba atarejesha wimbo kwenye akaunti yake ya youtube wakati huu uongozi upo kwenye mazungumzo na Eddy Yawe kutafuta suluhu ya mgogoro ulioibuka katika yao.
Utakumbuka kipindi cha nyuma Eddy Yawe walizozana na Carol Nantogo kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao Tukigale ambapo aliweza kumpokonya mrembo huyo hakimiliki zote za wimbo huo.