You are currently viewing EDWIN SIFUNA AMVUA NGUO BAHATI BILA HURUMA, ADAI THAMANI YAKE NI KSH. 200.

EDWIN SIFUNA AMVUA NGUO BAHATI BILA HURUMA, ADAI THAMANI YAKE NI KSH. 200.

Katibu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amepuzilia mbali madai yaliyoibuliwa na staa wa muziki nchini Bahati kuwa alihongwa shillingi millioni 50 kujiondoa kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare.

Mwanasiasa huyo amesema madai ya Bahati ambaye ni mchanga kisiasa hayana ukweli wowote, hivyo msanii huyo anatumia mgogoro uliopo kati yake na chama cha Jubilee kutafuta uhuruma kutoka kwa wakenya.

“Yaani kama kuna mtu ako na KSh 50 million mahali eti anataka kuchukua apee Bahati, huyo mtu kichwa yake ni mbaya. Afanyie nini? Ya nini?” Amesema Sifuna.

Sifuna alienda mbali na kumtolea uvivu Bahati kwa kusema kwamba pesa ambazo hitmaker huyo wa “Adhiambo” anapaswa kupewa ili ajiondoe kwenye azma yake kuwa mbunge Mathare ni shilingi mia 2.

“Hapo naweza chukua mia mbili nimbuyie nayo handkerchief nibaki an hiyo pesa ingine kwa sababu ya machozi alafu nimlipie salon ya mwaka moja hiyo nywele yake. Hakuna kitu ingine ya kumpatia.” Amekazia Sifuna.

Kauli ya Edwin Sifuna imekuja mara ya Bahati kumtuhumu kuwa amekuwa kizingiti kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa Mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 Mwaka huu.

Bahati alienda mbali na kudai kuwa Sifuna ndio alichochea chama cha Jubilee kumuondoa kama mperusha bendera ya ubunge wa Mathare kupitia Muungano wa Azimio la Umoja ili kumpa nafasi mbunge wa sasa Anthony Oluoch.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke