Mwanamuziki kutoka nchini Uingereza Edy Sheeran ametangaza kunasa virusi vya Covid-19 ikiwa ni siku chache zimebaki kabla ya kuachia Album yake ya nne inayokwenda kwa jina la Equals
Edy Sheeran ametoa taarifa hiyo kupitia ukursa wake wa Instagram ambapo ameandika “Ndugu zangu ningependa kuwajuza kuwa nimepimwa na kukutwa na Covid-191. Kwa hiyo kwa sasa nimejitenga kama vile utaratibu wa serikali unavyosema. Hii inamaana kuwa kwa sasa siwezi kufanya mambo yangu binafsi. Kwahiyo nitafanya mahojiano na kutumbuiza nikiwa nyumbani. Naomba radhi kwa yeyote niliyemkwaza”