Tajiri namba moja duniani na mmiliki wa mtandao wa Twitter, Elon Musk ameeleza kwamba Kampuni ya Apple inatishia kuizuia Twitter kupatikana kwenye App Store.
Musk ambaye aliinunua Twitter kwa zaidi ya KSh. Trilioni 5, amesema Apple hawajatoa sababu za kwanini wanataka kufikia uamuzi huo.
Wiki iliyopita Elon Musk alidokeza kwamba kama Apple watachukua maamuzi hayo ya kuifungia Twitter, basi itakuwa nafasi nzuri ya kuleta simu zake mwenyewe.