Timu ya Taifa ya Senegal imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu kwenye hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia mwaka huu baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Ecuador katika mchezo wa mwisho wa kundi A
Matokeo hayo yameifanya Senegal kumaliza wa pili katika kundi hilo kwa kufikisha alama 6 nyuma ya Uholanzi waliomaliza wakiwa vinara na alama 7 baada ya kuwazaba wenyeji Qatar 2-0 katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Wakati huo huo Timu ya Taifa ya England imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Dunia kwa kuizaba Wales 3-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B
Mabao mawili ya Marcus Rashford na moja la Phil Foden yametosha kuipa alama zote tatu England na kumaliza vinara kwenye msimamo wa kundi hilo kwa kufikisha alama 7
Sasa England atakutana na wawakilishi wa Afrika timu ya Taifa ya Senegal kwenye hatua ya 16 bora