EP mpya ya msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz, “First of All” inaendelea kufanya vizuri kupitia digital platforms mbalimbali.
Good news kwa upande wa Apple Music ni kwamba EP hiyo yenye jumla ya ngoma 10, ngoma zake zote zinashika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika orodha ya Top Songs Tanzania.
Nafasi ya kwanza imekamata wimbo uitwao “Melody” aliomshirikisha Jay Willz huku nafasi ya kumi ikishika kolabo yake na Mbosso, wimbo uitwao “Oka”.
Ikumbukwe EP hiyo ambayo haijamaliza siku tatu tangu iachiwe, imefanikiwa kupata mapokezi makubwa zaidi ndani ya saa chache.