You are currently viewing ERIC MONDI AFUNGUKA SABABU ZA KUMTEMA MSANII MISS P

ERIC MONDI AFUNGUKA SABABU ZA KUMTEMA MSANII MISS P

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi amefunguka sababu za kusitisha kufanya kazi na msanii Miss P baada ya kuchukua jukumu la kumsimamia.

Katika mahojiano na mungai Eve,  Omondi amesema changamoto kubwa ambayo kampuni yake ilikutana nayo kutoka kwa Miss P, ni msanii huyo kutoonyesha nia ya kutaka kuzisukuma  kazi zake za muziki  mwenyewe.

Mchekeshaji huyo amedai kuwa miss p hakuwa mtu wa kutumia mitandao ya kijamii na mara nyingi ilimbidi asitishe shughuli zake kwa ajili ya kusukuma muziki wa Miss P licha ya kutokuwa mwanamuziki.

Eric omondi amesema uzembe wa Miss P kusukuma muziki wake kama msanii ilichangia kampuni yake kuvunja mkataba wa kufanya nae kazi.

Kauli ya Eric Omondi imekuja siku chache mara baada ya Miss P kwenye mahojiano na mzazi willy tuva kudai kuwa aliacha kufanya kazi na eric omondi kwa sababu ni mtu haeleweki kwani alipoachia wimbo wake wa “Baby Shower” alikata mawasiliano nae.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke