Mchekeshaji Eric Omondi ameapa kwa kauli moja kuwa kabla ya mwaka huu kuisha mswada wake wa kucheza asilimia ya muziki wa Kenya kwenye vyombo vya habari utapatishwa kuwa sheria.
Katika mkao na wanahabari Omondi amesema kuanzia wiki ijayo atakita kambi nje ya majengo ya bunge kuhakikisha mswada huo unapitishwa kabla ya rais William Ruto kutia saini na kuwa sheria.
Aidha amepuzilia mbali madai ya baadhi ya wasaniii wanaodai kuwa anatumia maswada huo kutafuta kiki kwa kusema kuwa lengo lake kuuu ni kuleta mageuzi kwenye muziki wa Kenya ikiwemo wasanii kupewa kipau mbele kwenye matamasha ya muziki na nyimbo zao kupigwa kwenye vituo vya radio na runinga.
Utakumbuka tangu Eric Omondi aanzishe mjadala wa kuleta mageuzi kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya amepata ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu huku wakitamka akome kuingilia masuala ya wanamuziki wakati faini yake ni ucheshi.