Baada ya mchekeshaji Eric Omondi kukamatwa na kuachiwa uhuru akiwa kwenye harakati za kuwasilisha mswada bungeni wa kutaka asilimia 75 ya muziki wa Kenya upigwe kwenye vituo vya redio na runinga nchini, mchekeshaji huyo ameahapa kurejea tena bungeni.
Katika mkao na wanahabari Omondi amesema licha ya kwamba alipata changamoto kwenye jaribio lake la kwanza kufika bungeni, atafuata taratibu zote kisheria kuhakikisha kwamba mswada huo unawasilisha bungeni ambapo amedai ana imani kuwa wabunge watampitisha mswada huo bila pingamizi.
Omondi ameenda mbali zaidi na kusema kwamba amesikitishwa na hatua ya wasanii wa Kenya kususia maandamano ya kuwasilishwa mswada wa kuleta mabadiliko kwenye muziki wa kenya bungeni huku akidai kuwa kati ya wasanii 32 wenye mafanikio nchini ni wawili tu alijitokeza na kumuunga mkono kwenye azma yake hiyo.
Ikumbukwe kwa wiki moja sasa eric omondi amekuwa akitoa changamoto kwa wasanii wa Kenya kutia bidii kwenye kazi zao kwani muziki wa Kenya umeonekana kupoteza mweelekeo katika siku za hivi karibuni. Hii ni baada ya wasanii wa mataifa mengine kuonekana kupewa kipau mbele kufanya shows nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.