Mchekeshaji Eric Omondi amekanusha madai ya kutumia mjadala wa kuifufua muziki wa Kenya kujitafutia umaarufu.
Akipiga stori na podcast ya Captain Nyota Omondi amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa ana umaarufu mkubwa kuliko msanii yeyote hapa nchini huku akisisitiza kuwa anatumia ushawishi alionao kwa sasa kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Kenya ambao kwa mujibu wake umeshuka kwa asilimia kubwa.
Mchekeshaji huyo amesema wasanii wa Kenya hawana ubunifu kwenye uandaaji wa video zao za muziki kwa kuwa wameshindwa kutofautisha kati ya kuwa wabunifu na kiki, jambo ambalo amedai limewapelekea baadhi ya kuachia muziki usiokuwa na ubora.
Hata hivyo amewataka wasanii kujifunza kutoka kwa wasanii wa Nigeria na Tanzania ambao mara nyingi uwekeza pesa nyingi kwenye utayarishaji wa kazi zao kama njia moja wapo ya kuongeza nakshi kwenye nyimbo zao.