Mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi amekoshwa na kile kinachoendelea mtandaoni kati ya msanii Willy Paul na Jovial.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amewapongeza wawili hao kwa hatua ya kuhalalisha mahusiano mtandaoni kitendo ambacho amehoji ni ubunifu wa hali ya juu wa kutengeneza matukio yatakayowasaidia kutangaza muziki wao mtandaoni.
Mchekeshaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigana kwa udi na uvumba kutetea muziki wa Kenya, amesema kuwa kwa sasa ni vigumu kwa msanii kupata mafanikio makubwa pasi na kuwa na matukio yatakao mfanya awe gumzo kwa mashabiki zake.
Hata hivyo amewapa changamoto wasanii kuwa wabunifu ili kutengeneza maudhui ya burudani yatakayo jenga gumzo kwa mashabiki wao na kupitia njia hiyo wataweza kushinda na wasanii wa kimataifa.