Mchekeshaji Eric Omondi ameamua kumjibu Ringtone Apoko mara baada ya mwimbaji huyo kumkejeli kuwa ana mpango wa kumpa kazi ya shillingi Kshs.50,000 kwa mwezi.
Kwenye mahojiano na Ankaliray katika kipindi cha Uhondo wa Milele FM, Omondi amesema hawezi kataa ofa ya kuajiriwa na Ringtone ila ana shauku ni wapi haswa mwimbaji huyo atatoa pesa za kumudu mshahara wake ikizingatiwa kuwa kodi ya nyumba anayoishi ni shillingi 45,000 kwa mwezi.
Mchekeshaji huyo ameenda mbali na kudai kuwa Ringtone alifurushwa kwenye nyumba ya kifahari aliyokuwa akiishi mtaani Runda miezi sita iliyopita na sasa anaishi kwenye nyumba ya kupanga huko South C viungani mwa jiji la Nairobi.
“Mimi kazi sijakataa, ila nyumba hata hana. Kwani hujui stori ya Ringtone. Nyumba ali auctioniwa. Anaishi South C- mi si najua kwake. Analipa aje 50,000 na rent yake ni 45,000.” Alisema Eric Omondi.
Kauli ya Eric Omondi inakuja mara baada ya Ringtone kumtolea uvivu akiwa kwenye kipindi cha the Trend ya NTV ambapo alidai kuwa yupo tayari kumlipia mchekeshaji huyo shillingi 50,000 kwa mwezi kama mfanyikazi wake nyumbani ili aweze kumsaidia kufanya usafi kwenye mjengo wake wa kifahari huko mtaani Runda.