You are currently viewing ERIC OMONDI AMJIBU ZUCHU BAADA YA KUPINGA KAULI YAKE KUWA MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

ERIC OMONDI AMJIBU ZUCHU BAADA YA KUPINGA KAULI YAKE KUWA MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

Mchekeshaji Erick Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake kwamba muziki wa Bongofleva umekufa kufuatia baadhi ya wasanii wake kufanya Amapiano.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Omondi amemjibu Zuchu ambaye hakukubaliana na kauli hiyo akidai kwamba wanamuziki wa Tanzania wameamua kukumbatia muziki wa Amapiano ambao utawasaidia kujulikana zaidi.

“Bongofleva haiwezi kufa, wasanii wanatoka nje ya eneo lao, kutafuta utofauti wa kujaribu sauti mpya. haijawahi shuhudiwa ikiuua tasnia yoyote, tasnia ya muziki ni kubwa sana, acha msanii ajaribu mambo yake. Hayo ni mabadiliko” alisema Zuchu.

Kufuatia kauli hio Eric Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake huku akimjibu Zuchu na kumweleza kwamba wanamuziki wa Kenya walianza hivyo na muziki wao ukapotea

“Dada yangu mpendwa, hivi ndivyo inavyoanza, huwa tunaanza kwa kupoteza uhalisia na utambulisho wetu na kutoa visingizio vyake. Huku Kenya tulianza vivyo hivyo na Muziki wetu ukapotea”

“Bongofleva iko SAWAA kabisa na hakuna haja ya kuwaacha Bongo Fleva ati kwa ajili ya ‘diversify’ Amapiano ni Basi tu linapita ila sisi tundapanda bila kujua linaenda wapi, tutashindwa kurudi nyumbani.tutakuwa tunauza sera zao na kushindwa kurundi nyumbani. tutakuwa tunauza tamaduni zao na kuua zetu za nyumbani” Mchekeshaji Omondi alinakiri”

“Unapoimba ‘Sukari’ kwa sauti hiyo tamu ya kweli ya bongo na mdundo . unachofanya kimsingi ni kuinua na taifa na Bendera ya Tanzania”alisema Eric Omondi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke