You are currently viewing ERIC OMONDI AMVUA NGUO FEMI ONE, ADAI HANA JIPYA KWENYE TASNIA YA MUZIKI NCHINI KENYA

ERIC OMONDI AMVUA NGUO FEMI ONE, ADAI HANA JIPYA KWENYE TASNIA YA MUZIKI NCHINI KENYA

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi amemtolea uvivu staa wa muziki nchini Femi One hii ni baada ya mrembo huyo kumshtumu vikali kwa kauli aliyoitoa majuzi kuwa muziki wa Kenya umekufa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi ameshangazwa ni wapi Femi One ametoa nguvu ya kumshambulia ikizingatiwa kuwa amezembea kwenye suala la kuachia muziki mzuri kwani mara ya mwisho kuachia ngoma kali ilikuwa mwaka wa 2020 alipoachia singo iitwayo “Utaweza” akiwa amemshirikisha Mejja.

Haikushia hapo Eric Omondi ameenda mbali zaidi na kumtaka Femi One akubali kwamba kiwanda cha muziki nchini kimepoteza mweelekeo na badala yake aweke juhudi zaidi kwenye kazi zake kama njia moja ya kurejesha muziki wa Kenya katika ramani ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe juzi kati Eric omondi alisutwa vikali na wasanii wa Kenya kwa madai ya kuwavunjia heshima alipoibuka na kudai kwamba muziki wa Kenya umepoteza mvuto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke