You are currently viewing ERIC OMONDI AMVUA NGUO NOTI FLOW KWA KUMVUNJIA HESHIMA

ERIC OMONDI AMVUA NGUO NOTI FLOW KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi ameingia kwenye headlines mara baada ya kutupia maneno makali mtandaoni na rapa Noti Flow kuhusu magari waliyowanunulia wapenzi wao hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amemtaka Noti Flow kutofuatilia maisha yake ya ndani huku akitishia kumfundisha adabu pamoja na mpenzi wake King Alami.

“Ambie huyu CHOKORA Asiwahi Ita jina yangu tena!!!!  Ama nitamshika na huyu demu wake NIWAKULE mpaka wakue straight. IDIOT!!!!” Ameandika Omondi.

Post hiyo haikupokelewa vyema na Noti Flow ambaye alishuka kwenye uwanja wa comment ya post hiyo na kumchana tena Eric Omondi akisema mchekeshaji huyo amemkasirikia kwa sababu gari lake ni la kukodisha.

“He’s mad cz it’s car hire post logbook bruh. Chokora ni wewe na car hire zako. Clout chaser.” Ameandika Noti Flow.

Ikumbukwe purukushani kati ya Eric Omondi na Noti Flow ilianza mara baada ya mrembo huyo kumtaka Omondi aoneshe stakabadhi za gari aliyomnunulia mpenzi wake juzi kati ambapo alienda mbali na kujigamba kuwa tangu amnunulie gari mpenzi wake king alami mastaa wengi kutoka kenya wameanza kumuiga kwa kukodisha magari wakati hana lolote katika maisha.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke