You are currently viewing Eric Omondi amwagia sifa Vera Sidika kwa kiki ya kupunguza makalio

Eric Omondi amwagia sifa Vera Sidika kwa kiki ya kupunguza makalio

Mchekeshaji Eric Omondi ameamua kumpa maua yake akiwa hai mrembo Vera Sidika kwa kutengeneza tukio lilotikisa mitandao ya kijamii kabla ya kuachia wimbo wake mpya uitwao PopStar.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amelilinganisha tukio la Vera na matukio ya kusisimua ambayo wasanii wa Nigeria na Tanzania utengeneza kwa ajili ya kuteka hisia za mashabiki zao huku akimpongeza mrembo huyo kwa kuachia video kali yenye ubora tofauti na wasanii wa Kenya ambao wamekosa ubunifu kwenye kazi zao.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii wa Kenya hasa wa kike kuacha kulaza damu kwenye suala la kutengeneza matukio yatakayowasaidiwa kuzungumziwa mtandaoni na kwenye vyombo vya habari kama njia ya kuendana na nyakati zilizipo kwenye ulimwengu wa muziki.

Utakumbuka juzi kati Vera Sidika aliibuka na kukiri hadharani kupunguza makali yake kutokana athari za kiafya ambapo alienda mbali zaidi na kuwaonya watoto wa kike wasijaribu kubadilisha miili yao kwa njia ya upasuaji kwa kuwa ina madhara makubwa siku za mbeleni.

Hata hivyo baada ya kutikisa mitandao ya kijamii na taarifa yake hiyo alikuja akaachia wimbo wake mpya wenye mahadhi ya Hiphop, kitendo kilichowafanya walimwengu kuhoji kuwa alikuwa anatumia shepu yake kutafuta kiki ya kutangaza ujio wake mpya kwenye muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke