You are currently viewing ERIC OMONDI ATAKA WAKENYA KUSUSIA TAMASHA LA AFRO VASHA

ERIC OMONDI ATAKA WAKENYA KUSUSIA TAMASHA LA AFRO VASHA

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi amewataka wananchi wa kenya kususia tamasha ambalo limechapisha mabango au posters zenye picha ndogo za wasanii  wa Kenya huku yakiwa na picha kubwa za wasanii kutoka Tanzania.

Omondi ambaye amejinasibu kama mwanaharakati wa haki za wasanii wa kenya ameliita tukio hilo kama uvunjwaji wa heshima kwa masuper star wa Kenya huku akitoa muda kwa waandaaji wa mabango hayo kurekebisha la sivyo atahakikisha hakuna mtu atakae hudhuri tamasha la Afro vasha ambalo wasanii wa bongofleva harmonize na ali kiba watatumbuiza.

Kauli ya Eric Omondi imekuja mara baada ya bango la show ya Afro vasha ambalo litafanyika huko Naivasha desemba12  kuonyesha picha kubwa ya  wasanii hao wa bongo huku wasanii wakenya wakiweka kwenye picha ndogo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke