You are currently viewing ERIC OMONDI ATOA CHANGAMOTO KWA EZEKIEL MUTUA KUJA NA TUZO ZA MUZIKI NCHINI KENYA

ERIC OMONDI ATOA CHANGAMOTO KWA EZEKIEL MUTUA KUJA NA TUZO ZA MUZIKI NCHINI KENYA

Mchekeshaji Eric Omondi amemshauri mwenyekiti wa mwenyekiti mpya wa chama cha muziki kinachojihusisha na hakimiliki nchini Kenya Ezekiel Mutua kuja na tuzo za muziki kama ana nia njema ya kufufua muziki wa kenya ambao umeonekana kumpoteza mweelekeo katika siku za hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Omondi amesema kuandaliwa kwa tuzo hizo za  muziki itatoa nafasi ya kutambua mchango wa wasaniii wanaofanya vizuri kimuziki nchini,  jambo ambalo amedai litawafanya wasanii kurejesha imani kwa chama cha muziki kinachojihusisha na hakimiliki nchini.

Hata hivyo Eric Omondi amemtaka ezekiel mutua kuwekeza pesa nyingi kwenye suala la kurejesha tuzo za muziki nchini huku akipendekeza Julai 2 mwaka huu kama siku nzuri ambayo hafla ya ugawaji tuzo inapaswa kufanyika nchini.

“Daktari, Life rarely gives us a second chance but when it does then we are called upon to give it our very best. This is your chance to ABSOLVE yourself and here is how you can do it. Artists lost Faith in MCSK and this is a great paradox because if MCSK is here for the Artists and the Artists have no faith in it then it lacks PURPOSE,” amesema Eric Omondi

Mchekeshaji huyo ameongeza “HERE IS MY PROPOSAL TO YOU. Let us Establish a MUSIC AWARDS SHOW that will not only recognize but also Award Perfoming Artists. INJECT MONEY BACK INTO THE INDUSTRY.This will help bring back life into the Industry which is currently seriously lacking. July 2nd 2022 is my PROPOSED DATE. KAZI KWAKO!!!,”

Licha ya Eric Omondi kuwasilisha mapendekezo yake hayo kupitia mtandao wake wa Instagram Ezekiel Mutua ambaye ni mwenyekiti mpya wa chama cha muziki kinachojihusisha na hakimiliki nchini Kenya hajatoa tamko lolote kuhusu suala hilo ila ni jambo la kusubiriwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke