Mchekeshaji Eric Omondi amewashauri wanaume kutokumbatia mpango wa uzazi wa kukata mishipa ya uzazi maarufu kama Vasectomy.
Kwenye mahojiano na mpasho Omondi amesema hakubaliani na njia hiyo ya upangaji uzazi kwa kuwa inamzuia mwanaume kutekeleza wajibu wake wa kujaza dunia kwa kuzaa watoto wengi kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu.
Utakumbuka juzi kati msanii Bien wa Sauti Sol alikiri hadharani kuwa yupo tayari kumsaidia mke wake kupanga uzazi kwa njia ya kukata mshipa wake wa uzazi maarufu kama Vasectomy kwani wanaume wengi katika nchi za kiafrika wamewaachia akina mama jukumu hilo.