You are currently viewing ERIC OMONDI AWAPONDA WATAYARISHAJI WA YOUNG, FAMOUS & AFRICAN,ADAI WAMEMUIBIA UBUNIFU WAKE

ERIC OMONDI AWAPONDA WATAYARISHAJI WA YOUNG, FAMOUS & AFRICAN,ADAI WAMEMUIBIA UBUNIFU WAKE

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kudai kuwa waandaaji wa reality show ya Young, Famous & African waliiba ubunifu wa kipindi chake cha Wife Material.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchekeshi huyo ametilia shaka namna ambavyo maudhui ya show hiyo yenye matukio halisi ina fanana kwa asilimia 100 na ya kipindi chake cha Wife Material huku akisema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa watayarishaji wa Young, Famous & African waliiba mawazo yake.

Kwa upande wake mtayarishaji wa kipindi cha Wife Material mchekeshaji Eddie Butita amesema yuko tayari kufanya kazi na maprodyuza wa Young, Famous and African kama wataonyesha nia ya kuhitaji huduma zake.

Kauli yao Eric Omondi imekuja mara baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini kuzua mjadala na kuhoji ni kwa nini mastaa wa Kenya hawakuhusishwa kwenye show ya Young, Famous and African ambapo wengi walihoji huenda kiburi ndio imewaponza mastaa wengi wa Kenya.

Utakumbuka Show ya Young, Famous & african ilianza kuruka kwenye mtandao wa Netflix, Machi 18, 2022 kupitia maonyesho saba yaliyowashirikisha mastaa wakubw, kutoka Afrika kusini, Uganda, Tanzania, na Nigeria ambapo kwa Afrika Mashariki tunawakilishwa na Diamond Platinumz pamoja na Zari TheBossLady.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke