You are currently viewing ERIC OMONDI AWATOLEA UVIVU WASANII TANZANIA, ADAI MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

ERIC OMONDI AWATOLEA UVIVU WASANII TANZANIA, ADAI MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

Baada ya kuuzungumzia sana muziki wa Kenya kiasi cha kukamatwa na polisi , akidai kuwa muziki Kenya unakufa na wasanii wake hawajitumi, mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi ameugeukia muziki wa Bongofleva na wasanii wake akidai muziki wa amapiano unaua utambulisho wa muziki wa Bongofleva kutoka Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchekeshaji huyo mwenye zaidi ya wafuasi million 3.7 ameeleza kuwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki muziki wa bongofleva ndio ulikuwa kama utambulisho wa Ukanda huu lakini kwa kuiga muziki wa Amapiano ,muziki wa bongo fleva umepotea.

Omondi amewataka wasanii wa Tanzania kuamka na kurudi katika utambulisho wao wa Bongofleva huku akidai kuwa wakenya wamelala , na inafaa watanzania warejee kwa upesi kwenye muziki wao kabla ya muda kuisha.

EAST AFRICA I am SAD!!! I Weep for my PEOPLE😥😥😥. Nina Huzuni Moyoni😥. Bongo flava has always been East Africa’s PRIDE ila Kwa sasa IMEKUFAA. Kila Tanzania Artist Kwa sasa Anaimba Amapiano. We have lost our CULTURE, Killed our Own!!! Tumekaribisha, tumeiga, tumeichukua Tabia na Mwenendo zake Jirani tukajisahau wenyewe😥😥😥. We are LOSING OUR IDENTITY, OUR PRIDE!!! Naomba ndugu Zangu Wa BONGO Turejee kwa upesi before it’s too late!!! Wakenya WAMELALA, Wa Tanzania WAMEJIPOTEZAA. Mungu TUHURUMIE, TUREHEMU🙏🙏😥😥…aliandika Omondi kupitia Instagram yake

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke