You are currently viewing ERIC OMONDI AZIDI KUANIKA MADHAIFU YA WASANII WA KENYA

ERIC OMONDI AZIDI KUANIKA MADHAIFU YA WASANII WA KENYA

Mchekeshaji Eric Omondi amekuwa akichefukwa na Kiwanda cha Muziki nchini Kenya, leo ameibuka tena baada ya Diamond Platnumz kutumbuiza kwenye hafla ya mwisho ya mkutano wa kisiasa wa Azimio la Umoja One Kenya katika uwanja wa Kasarani ambapo inadaiwa Chibu alilipwa kiasi cha Ksh. Millioni 10 kutumbuiza kwa dakika 30 tu.

Eric Omondi ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigana kwa udi na uvumba kutetea muziki wa humu nchini huku akitamba taasisi zote na washikadau kukumbatia kucheza miziki ya Kenya kwa asilimia 75, alisema kwamba hana ubaya na Diamond Platnumz ila inasikitisha sana kwamba katika halfa ya kihistoria kama ile ya Kasarani, hakuna msanii hata mmoja wa humu nchini alipata kutambulika na kuoenekana kuwa wa thamani.

Mchekeshaji huyo alionekana kuwalaumu wasanii wa Kenya kwa kutojijenga vizuri na kujikuza (SHOWBIZ) kwa njia inayoweza kuwapeleka kwenye majukwaa makubwa na ya kihistoria kama hayo. Omondi alitolea mfano kwa kuweka orodha ya wasanii wanaosikilizwa zaidi Kenya ambapo Top 5 wamekaa wasanii wa Tanzania.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke