Mchekeshaji mashuhuri nchini Eric Omondi amezua gumzo mtandaoni baada ya kudai kuwa anatarajia mtoto pamoja na mwanamuziki Miss P.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram omondi ameshare picha inayomuonyesha Miss P akiwa mjamzito na kumhakikishia kuwa atawajibikia mahitaji ya mtoto wao ajaye ikizingatiwa kuwa watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.
Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamoo wakiwemo mastaa wenzake wamejitokeza na kuwapongeza wawili hao huku wengine wakidai kuwa ujauzito huo si wa kweli kwani ni kiki tu wanatafuta.
Taarfa za chini ya carpet zinasema kwamba Miss P yupo mbioni kuachia singo yake mpya hivi karibuni na ndio maana amehamua kutumia madai ya ujauzito kutafuta kiki. Eric Omondi si mgeni kwa drama na anajulikana kuwa mbunifu sana katika utafutaji wa kiki.