You are currently viewing ERIC OMONDI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUKWEPA KULIPA DENI.

ERIC OMONDI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUKWEPA KULIPA DENI.

Mchekeshaji Eric Omondi anatarajiwa kufikisha kortini Mei 27 mwaka huu kwa tuhuma za kukwepa kulipa deni la shillingi la 4 za Kenya.

Taarifa hiyo imethibitisha na mwanamitindo wa masuala ya urembo nchini Melina kwenye mahojiano na Presenter Ali ambapo amesema kwamba mchekeshaji huyo ameshindwa kuheshimu agizo la mahakama la kumlipa deni lake kwa awamu mbili.

Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba amesikitishwa na kitendo cha Omondi kukwepa simu zake kila mara anapojaribu kumuulizia kuhusu deni hilo jambo analosema limemlazimu kufufua tena kesi lilokuwa linamuandama.

Hata hivyo amesema hatalegeza msimamo wa kumchukulia Omondi hatua kali za kisheria na ana Imani mahakama itamtendea haki ili iwe funzo kwa wanaokimbia madeni ya watu.

Utakumbuka Melina amekuwa akimvalisha Eric Omondi kwenye shughuli zake lakini mchekeshaji huyo aliingiwa na jeuri baada ya kushindwa kulipa huduma aliyopewa na mrembo huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke