Baada ya kuwatolea uvivu wasanii wa Kenya kwa kufelisha kiwanda cha muziki, Mchekeshaji maarufu Eric Omondi ameibuka na jambo lingine, amehapa kuwasilisha hoja bungeni wiki ijayo , hoja ambayo inalenga kuhimarisha muziki wa Kenya .
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi mswaada huo unalenga kushinikiza asilimia 70 ya nyimbo za wasanii wa wakenya zinachezwa kwenye vituo vya redio na runinga.
Mchekeshaji huyo ameenda mbali zaidi na kusemba kwamba vyombo vya habari nchini Kenya vimekuwa vikitangaza sana nyimbo za wasanii wa nje, jambo ambalo amedai kwamba lilipelekea muziki wa Kenya kukosa thamani.
Hata hivyo Eric omondi amewataka wasanii wa Kenya kuungana nae wiki ijayo kuwasilisha hoja hiyo bungeni huku akiwataka wabunge vijana kama Babu Owino na Charles Njagua kuwasaidia kuusukuma mswaada huo la sivyo ataanzisha harakati ya kuwaangusha kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2021.
Ikumbukwe kwa wiki moja sasa Eric Omondi amekuwa akitoa changamoto kwa wasanii wa Kenya kutia bidii kwenye kazi zao kwani muziki wa Kenya umeonekana kupoteza mweelekeo katika siku za hivi karibuni. Hii ni baada ya wasanii wa mataifa mengine kuonekana kupewa kipau mbele kufanya shows nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.