You are currently viewing ERIC OMONDI NA BIEN WA SAUTI SOL WARUSHIANA MAKONDE KWENYE ONESHO LA KONSHENS

ERIC OMONDI NA BIEN WA SAUTI SOL WARUSHIANA MAKONDE KWENYE ONESHO LA KONSHENS

Mchekeshaji Eric Omondi ameingia kwenye headlines baada ya kutaka kuzichapa na member wa Sauti Sol, Bien baraza usiku wa kuamkia Januari mosi katika onesho la Konshens Jijini Nairobi.

Chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Omondi kushinikiza kundi la Sauti Sol watumbuize wa mwisho katika orodha ya wasanii kama njia ya kuwapa heshima.

Làkini Pia Bien katika moja ya interview amenukuliwa akisema muda wanaopewa kuperfom kama kundi la Sauti Sol katika tamasha haijawahi kuwa tatizo kwao, iwapo atakuwa wasanii wa kwanza au wa mwisho katika orodha ya wasanii.

Ikumbukwe kwa muda  sasa eric omondi amekuwa akipaza sauti juu ya wasanii wa kenya kutotendewa haki na waandaaji wa matamasha ya muziki.

Hii ni baada ya wasanii wa mataifa mengine kuonekana kupewa kipau mbele kufanya shows nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke